IMEANDALIWA NA MPISHI Rahma @http://jinsiyakupika.com
jinsi ya kuandaa Kachumbari mchanganyiko: Habari mpenzi wa blogu yetu, Leo tunakuletea namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko. Fuatana nami
Namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko hatua kwa hatua
Mahitaji muhimu
Nyanya kubwa 2
Vitunguu maji 3
Karoti 3
Pili pili hoho ya kijani 1
pilipili hoho nyekundu 1
Tango 1
Kotmiri 1/2
fungu(1/2 kicha ) au 1/2 bunch
Majani ya Iliki (parsley) 1/2 fungu (1/2 kichana) au 1/2 bunch
Cerely vijiti 4
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Jinsi ya kuandaa/kutayarisha
Osha mbogamboga kwa kutumia maji safi ya uvugu vugu (pendelea kuosha saladi kwa kutumia maji ya namna hii ili kuua vijidudu)
Katakata vitu vyote isipokuwa ndimu, kisha uweke katika mashine ya kusagia chakula (yaani food processor)
Weka namba mbili kwenye mashine yako kisha Saga mchanganyiko wako kwa kusita sita kila baada ya sekunde 1 mpaka kachumbari yako ichanganyike vizuri.
Ikishachanganyika vizuri, Weka maji ya ndimu kisha changanya na kijiko, Tia ndani ya bakuli tayari kwa kuliwa
Vilevile waweza kutumia brenda kwa ajili ya kusagia, hakikisha usisage kwa muda mrefu ili isiwe majimaji sana. Hivyo ndio namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko. Asanteni!
No comments:
Post a Comment