Picha ndo radha halisi
ya Facebook. Bila ma picha picha hautaona kitu bali
mahabari ya siasa, mara nani kafanya nini au maelezo yasiyotuhusu, hakuna anaeingia
facebook kusoma novel, hadithi au habari zisizomhusu bhana! Ila picha! Picha
zina amsha amsha facebook – la hasha hatuna mbaya na jamaa yako anaepost habari
flani zisizotuhusu kila saa.
Ingawa hata ukitupia picha facebook bila
mpangilio bado utawavutia marafiki zako, lakini mbona bado sio kazi, chukua
muda wako mchache tu kupangilia maingizo ya picha zako ili kuvutia marafiki
zako zaidi na zaid.
Kuna njia kama tatu hivi za msingi kufikiria
katika kuedit picha za facebook.
Moja;
ni katika uchaguzi wa picha gani iingie kwenye ukurasa yako wa facebook, ya
pili ni kutumia software / programu maalum za kuboreshea picha na ya tatu I
kuweka mpangilio ambao utavuta na kua bora kutazamwa na marafiki wa kila aina.
Tuanze na kipengele cha kwanza – kuchagua aina
za picha za kutupia facebook. Hiki ni kipengele rahisi zaidi. Kwanza usiweke
picha yoyote ambayo unafikiri wewe mwenyewe usingependa kuiona au watu flani
hawata penda kuona.kua mwangalifu juu ya aina ya picha unazotaka kushare na
usijidhalilishe wewe au marafiki zako; vinginevyo utapoteza baadhi ya marafiki.usiboe
watu kwa kutupia picha hamsini za mbwa wenu mbaya mmoja akijisaidia. Usiweke
picha za ngono.
Na tukija kwenye suala la ku edit picha
zenyewe, una mambo kadha wa kadha ya kuchagua;
Ø Kuna programu nyingi za bure mtandaoni
unazoweza kutumia kama utakavyojifunza kwenye
makala zinazokuja.
Ø Kama bajeti inaruhusu wape kazi wataalamu wa kuedit picha, sio mbaya.
Mwisho, mtandao wa facebook unakupa njia
kadhaa za kupangilia picha zako, kwa mfano unaweza kuweka picha katika albam
tofauti tofauti. Kurahisisha upatikanaji wa picha zako, zipange kwa matukio,
kwa mfano. Mkesha wa krismasi, mwaka mpya au serengeti tour.
No comments:
Post a Comment