KARIBU

tujifunze pamoja jinsi ya kufanya mambo mbalimbali; +255 758100222, tuma maoni, omba mada, dhamini mtando n.k jinsiya.tz@gmail.com

Monday, 6 February 2017

PICHA: JINSI YA KUFUNGA TAI

hii ni style ya kiingereza zaidi, na inafaa ofisini na katika tafrija mbalimbali, hii ni staili pekee ambayo kila mwanaume anapaswa kuifahamu;


Friday, 31 January 2014

JINSI YA KUANDAA KACHUMBARI MCHANGANYIKO

IMEANDALIWA NA MPISHI Rahma @http://jinsiyakupika.com jinsi ya kuandaa Kachumbari mchanganyiko: Habari mpenzi wa blogu yetu, Leo tunakuletea namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko. Fuatana nami Namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko hatua kwa hatua
Mahitaji muhimu
Nyanya kubwa 2
Vitunguu maji 3
Karoti 3
 Pili pili hoho ya kijani 1
pilipili hoho nyekundu 1
Tango 1
Kotmiri 1/2
fungu(1/2 kicha ) au 1/2 bunch Majani ya Iliki (parsley) 1/2 fungu (1/2 kichana) au 1/2 bunch
 Cerely vijiti 4
 Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Jinsi ya kuandaa/kutayarisha 
Osha mbogamboga kwa kutumia maji safi ya uvugu vugu (pendelea kuosha saladi kwa kutumia maji ya namna hii ili kuua vijidudu) Katakata vitu vyote isipokuwa ndimu, kisha uweke katika mashine ya kusagia chakula (yaani food processor)

Weka namba mbili kwenye mashine yako kisha Saga mchanganyiko wako kwa kusita sita kila baada ya sekunde 1 mpaka kachumbari yako ichanganyike vizuri.

Ikishachanganyika vizuri, Weka maji ya ndimu kisha changanya na kijiko, Tia ndani ya bakuli tayari kwa kuliwa Vilevile waweza kutumia brenda kwa ajili ya kusagia, hakikisha usisage kwa muda mrefu ili isiwe majimaji sana. Hivyo ndio namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko. Asanteni!

Wednesday, 15 January 2014

JINSI YA KUPATA MIMBA YA MTOTO WA KIUME



Kupata mtoto wa kiume ni jambo muhimu sana kwa baadhi ya wazazi. Ndio maana kwa njia yoyote ile wengi hufanya juu chini kufanikisha jambo hili, wengine hudiriki kwenda kwa waganga wa kienyeji na wenye imani zao kusali sana. Lakini kitaalamu hii inaitwa uchaguzi wa jinsia *gender selection. Na inaweza kufanyika kwa mtoto wa kike au wa kiume, Ingawa kupata mimba ya mtoto wa kiume mara nyingi ni tofauti kidogo.

JINSI YA KUPANGILIA PICHA, KUPENDEZESHA PROFILE ZA FACEBOOK



Picha ndo radha halisi ya  Facebook. Bila ma picha picha hautaona kitu bali mahabari ya siasa, mara nani kafanya nini au maelezo yasiyotuhusu, hakuna anaeingia facebook kusoma novel, hadithi au habari zisizomhusu bhana! Ila picha! Picha zina amsha amsha facebook – la hasha hatuna mbaya na jamaa yako anaepost habari flani zisizotuhusu kila saa.