KARIBU

tujifunze pamoja jinsi ya kufanya mambo mbalimbali; +255 758100222, tuma maoni, omba mada, dhamini mtando n.k jinsiya.tz@gmail.com

Wednesday, 15 January 2014

JINSI YA KUPATA MIMBA YA MTOTO WA KIUME



Kupata mtoto wa kiume ni jambo muhimu sana kwa baadhi ya wazazi. Ndio maana kwa njia yoyote ile wengi hufanya juu chini kufanikisha jambo hili, wengine hudiriki kwenda kwa waganga wa kienyeji na wenye imani zao kusali sana. Lakini kitaalamu hii inaitwa uchaguzi wa jinsia *gender selection. Na inaweza kufanyika kwa mtoto wa kike au wa kiume, Ingawa kupata mimba ya mtoto wa kiume mara nyingi ni tofauti kidogo.



Jambo hili sio jipya sana katika jamii zetu lilifanywa toka enzi za mababu zetu. Zamani jambo hili liliangaliwa sana na wanawake kwa sababu haikueleweka kwamba mwanaume anahusika zaidi katika jambo hili. Lakini sasa kulingana na kukua kwa teknolojia na busara wanaume wanahusika zaidi, licha ya kua imani kama madawa ya kienyeji na mila bado zinaendelea.
Lengo la kuchagua jinsia ya kijacho limekua likikua siku hadi siku, baadhi ya watafiti wameonyesha asilimia 90 ya wazazi wamesema wangependa kuchagua jinsia kama ingekua rahisi. Matakwa ya mtoto wa kike au wa kiume yamekua yakitofautiana kulingana na maeneo.
Jinsi ya kuchagua mtoto  wa kiume
Kila mzazi huchangia nusu ya virutubishi vinavyounda mtoto. Kibaiolojia mama anamayai aina XX, kwa hiyo kama atachangia yai moja ili kupata mtoto, anao uwezo wa kuchangia yai X tu. Baba ana mayai  XY na kama atachangia kuunda mtoto, anaweza kuchangia yai X au yai Y. Hii inamaanisha shahawa/ mayai ambayo wazazi watachangia ndio huamua jinsia gaani mtoto atatokea.
Mama akitoa X na baba X = XX (mtoto wa kike)
Mama akitoa X na baba Y = XY (mtoto wa kiume)
Kama mama  anaouwezo wa kuchangia yai X tu ina maana swala ni baba atoe yai Y iwe XY ili kupata mtoto wa kiume. Kama ni hivyo usije ukadhani swala hilo ni juu ya baba peke yake, inahitaji ushirikiano kufanikisha jambo hilo, kama nitakavyo ainisha hapa chini;
Zaidi ya shahawa milioni mia mbili huingia ukeni mwanaume akikojoa/ piga bao mara moja, ikiwa ni mchanganyiko wa mayai X na Y. Lakini mara nyingi kati ya shahawa hizo milioni mia mbili, ni moja tu hupenya mpaka kwenye mfuko wa uzazi ili kukutana na yai la mama na kuunda mimba, nyingine ni uchafu na hutoka mwanamke akisafisha uke.
Kabla haujajua chakufanya ili kufanikisha zoezi la kupata mtoto wa kiume zijue sifa za shahawa, X na Y ambazo baba anaweza kuzalisha.
Shahawa X ina spidi ndogo ukilinganisha na Y lakini inauwezo wa kuishi muda mrefu zaidi kusubir yai la mama kama lilikua halijafika kwenye mfuko wa uzazi bado.
Shahawa Y ina speed kali zaidi kushinda X kuelekea kwenye mfuko wa uzazi llakini haina uwezo wa kuishi muda mrefu zaidi kama yai la mama litachelewa kufika kwenye mfuko wa uzazi.
Hivyo basi, ili kupata mtoto wa kiume inabidi ujifunze utaalamu wa kuvizia au kupanga jinsi gani ufanye ili wakati yai la mama linapofika kwenye mfuko wa uzazi likutane na shahawa Y ya baba kabla haijafa……..
Nini kifanyike;
Lenga kujamiiana masaa 24 kabla, mpaka 12 baada ya yai la mama kufika kwenye mfuko wa uzazi. Hii inamaanisha wakati yai la mama linafika katika mfuko wa mama inatakiwa kuwe na shahawa Y kwa wingi au kusiwe na shahawa kabisa lakini mara tu baada ya kufika kwa yai, mama anatakiwa kujamiiana ili kupanda shahawa nyingi ambazo ni Y kama nilivyokwambia shahawa Y zina spidi sana hivyo ni rahisi kuwahi na kulikuta yai pale.

Jinsi ya kufanikisha hilo;

·         Kwanza mwanamke aujue vizuri mzunguko wake wa mwezi, anaweza kwenda vituo vya afya kuelekezwa vizuri jinsi ya kuuelewa mzunguuko wake wa mwezi(hedhi) 

·         Baada ya kuuelewa vizuri mzunguko huo, yuko tayar kwa uwindaji wa jambo hili. Baada ya kutoka hedhi siku kama tatu hadi tano yai jingine huwa limefika kwenye mfuko wa uzazi kusubiri kurutubishwa. Ina maana baada ya kutoka hedhi subiri kwa siku 4 hadi tano kabla ya kujamiiana.

·         Mwanaume hatakiwi kua amepiga bao kwa njia yoyote siku 4-5 kabla ya kujamiiana siku mliyopanga.

  
·         Huwa kuna mabadiliko ya joto la mwanamke kujua kama yai limeshafika kwenye mfuko wa uzazi, ni vyema kama umeuelewa vizur mfumo wako wa uzazi wa mwezi uweze kujipima na kujua wakati yai la mwanamke limefika kwenye mfuko. Ukiweza jambo hilo ni vyema zaidi basi na mjitahidi kujamiiana  masaa kumi na mbili baada ya yai kufika kwenye mfuko.

·         Kaeni mikao ya kuhakikisha uume umeingia ndani sana ili kupunguza umbali wa shahawa kusafiri.

·         Ni muhimu mwanamke aandaliwe vizuri ili akojoe/afike kileleni kwa sababu shahawa za mwanamke husaidia kusafirisha mayai ya mwanaume.
Mlo.
Tunaamini pia mlo unaopata husaidia sana kukufanya upate mtoto wa kike au wa kiume, ili kupata mtoto wa kiume vyakula vifuatavyo husaidiia:
·         Nyama, hasa nyama nyekundu.
·         Vyakula vya chips chips zenye chumvi
·         Mayai, maharagwe,mikate na mazao ya mahindi
·         Caffeine; umhimize mwenza wako kunywa vinywaji vyenye caffeine kama koka na pepsi kabla ya kujamiiana kwa sababu vinasaidia kuchangamsha shahawa Y
·         Kunywa dawa ya kikohozi kabla ya kujamiiana kwa sababu dawa hizo huwa na guaifenesin   inayosaidia nguvu za usafirishwaji wa shahawa Y. soma juu ya dawa kuhakikiasha ina guaifenesin  kabla ya kunywa.
Mambo mengine yanayoweza kusaidia;
·         Mwanaume afike kileleni/akojoe kwanza.
·         Mwanaume awe juu au akae
·         Mjamiiane huku mmesimama
·         Mjamiiane usiku.
·         Epuka kujamiiana wakati mwezi unatoka au wakati wa mwezi mzima, fanya mwezi ukiwa robo zaidi.



9 comments:

  1. naomba msaada mm mwezi ulio pita nimeanza ku bleed tarehe6 na huwa nableed kwa cku nne na mwezi huu nimeanza kubleed leo tarehe 30 kwamahesabu hayo mm lini naweza kupata mtoto wa kiume ndani ya mwezi huu cku yangapi

    ReplyDelete
  2. Asante kwa maerezo hayohayoooo.������������


    ReplyDelete
    Replies
    1. natamani mungu aje anijalie mtoto wa kiume

      Delete
  3. Mbona kupata mtoto wa kiume masharti mengi sana

    ReplyDelete
  4. mie hata sielewi kwa kuwa nyama kahawa soda utajazo vyote ni tindikali. na yai y husafiri zaidi kwenye nyongo ( alkaline)
    alafu siku ulivyozipanga sijaelewa nisaidie hapo

    ReplyDelete
  5. Aki natamani Sana kupata Moto wa kiume,lakini nashindwa kuelewa exactly that date,please help me to know .

    ReplyDelete
  6. Hii imekaa vizuri Sana.
    I'aeleweka .

    ReplyDelete
  7. Nafaa kufanya nin ilikupata mtoto wa kiume

    ReplyDelete