
Kupata mtoto wa kiume ni jambo muhimu sana kwa
baadhi ya wazazi. Ndio maana kwa njia yoyote ile wengi hufanya juu chini
kufanikisha jambo hili, wengine hudiriki kwenda kwa waganga wa kienyeji na
wenye imani zao kusali sana. Lakini kitaalamu hii inaitwa uchaguzi wa jinsia
*gender selection. Na inaweza kufanyika kwa mtoto wa kike au wa kiume, Ingawa
kupata mimba ya mtoto wa kiume mara nyingi ni tofauti kidogo.
Jambo hili sio jipya sana
katika jamii zetu lilifanywa toka enzi za mababu zetu. Zamani jambo hili
liliangaliwa sana na wanawake kwa sababu haikueleweka kwamba mwanaume anahusika
zaidi katika jambo hili. Lakini sasa kulingana na kukua kwa teknolojia na
busara wanaume wanahusika zaidi, licha ya kua imani kama madawa ya kienyeji na
mila bado zinaendelea.
Lengo la kuchagua jinsia
ya kijacho limekua likikua siku hadi siku, baadhi ya watafiti wameonyesha
asilimia 90 ya wazazi wamesema wangependa kuchagua jinsia kama ingekua rahisi. Matakwa
ya mtoto wa kike au wa kiume yamekua yakitofautiana kulingana na maeneo.
Jinsi ya kuchagua
mtoto wa kiume
Kila mzazi huchangia nusu
ya virutubishi vinavyounda mtoto. Kibaiolojia mama anamayai aina XX, kwa hiyo
kama atachangia yai moja ili kupata mtoto, anao uwezo wa kuchangia yai X tu. Baba
ana mayai XY na kama atachangia kuunda
mtoto, anaweza kuchangia yai X au yai Y. Hii inamaanisha shahawa/ mayai ambayo
wazazi watachangia ndio huamua jinsia gaani mtoto atatokea.
Mama akitoa X na baba X =
XX (mtoto wa kike)
Mama akitoa X na baba Y =
XY (mtoto wa kiume)
Kama mama anaouwezo wa kuchangia yai X tu ina maana
swala ni baba atoe yai Y iwe XY ili kupata mtoto wa kiume. Kama ni hivyo usije
ukadhani swala hilo ni juu ya baba peke yake, inahitaji ushirikiano kufanikisha
jambo hilo, kama nitakavyo ainisha hapa chini;
Zaidi ya shahawa milioni
mia mbili huingia ukeni mwanaume akikojoa/ piga bao mara moja, ikiwa ni
mchanganyiko wa mayai X na Y. Lakini mara nyingi kati ya shahawa hizo milioni
mia mbili, ni moja tu hupenya mpaka kwenye mfuko wa uzazi ili kukutana na yai
la mama na kuunda mimba, nyingine ni uchafu na hutoka mwanamke akisafisha uke.
Kabla haujajua chakufanya
ili kufanikisha zoezi la kupata mtoto wa kiume zijue sifa za shahawa, X na Y
ambazo baba anaweza kuzalisha.
Shahawa X ina spidi ndogo ukilinganisha na Y lakini inauwezo wa kuishi muda mrefu
zaidi kusubir yai la mama kama lilikua halijafika kwenye mfuko wa uzazi bado.
Shahawa Y ina speed kali zaidi kushinda X kuelekea kwenye mfuko wa uzazi
llakini haina uwezo wa kuishi muda mrefu zaidi kama yai la mama litachelewa
kufika kwenye mfuko wa uzazi.
Hivyo basi, ili kupata
mtoto wa kiume inabidi ujifunze utaalamu wa kuvizia au kupanga jinsi gani
ufanye ili wakati yai la mama linapofika kwenye mfuko wa uzazi likutane na
shahawa Y ya baba kabla haijafa……..
Nini kifanyike;
Lenga kujamiiana masaa 24 kabla, mpaka 12 baada ya yai la mama
kufika kwenye mfuko wa uzazi. Hii inamaanisha wakati yai la mama linafika
katika mfuko wa mama inatakiwa kuwe na shahawa Y kwa wingi au kusiwe na shahawa
kabisa lakini mara tu baada ya kufika kwa yai, mama anatakiwa kujamiiana ili
kupanda shahawa nyingi ambazo ni Y kama nilivyokwambia shahawa Y zina spidi
sana hivyo ni rahisi kuwahi na kulikuta yai pale.
Jinsi ya kufanikisha hilo;
·
Kwanza mwanamke aujue vizuri mzunguko wake wa mwezi, anaweza
kwenda vituo vya afya kuelekezwa vizuri jinsi ya kuuelewa mzunguuko wake wa
mwezi(hedhi)
·
Baada ya kuuelewa vizuri mzunguko huo, yuko tayar kwa uwindaji
wa jambo hili. Baada ya kutoka hedhi siku kama tatu hadi tano yai jingine huwa
limefika kwenye mfuko wa uzazi kusubiri kurutubishwa. Ina maana baada ya kutoka
hedhi subiri kwa siku 4 hadi tano kabla ya kujamiiana.
·
Mwanaume hatakiwi kua amepiga bao kwa njia yoyote siku 4-5 kabla
ya kujamiiana siku mliyopanga.
·
Huwa kuna mabadiliko ya joto la mwanamke kujua kama yai
limeshafika kwenye mfuko wa uzazi, ni vyema kama umeuelewa vizur mfumo wako wa
uzazi wa mwezi uweze kujipima na kujua wakati yai la mwanamke limefika kwenye
mfuko. Ukiweza jambo hilo ni vyema zaidi basi na mjitahidi kujamiiana masaa kumi na mbili baada ya yai kufika
kwenye mfuko.
·
Kaeni mikao ya kuhakikisha uume umeingia ndani sana ili
kupunguza umbali wa shahawa kusafiri.
·
Ni muhimu mwanamke aandaliwe vizuri ili akojoe/afike kileleni
kwa sababu shahawa za mwanamke husaidia kusafirisha mayai ya mwanaume.
Mlo.
Tunaamini pia mlo
unaopata husaidia sana kukufanya upate mtoto wa kike au wa kiume, ili kupata
mtoto wa kiume vyakula vifuatavyo husaidiia:
·
Nyama, hasa nyama nyekundu.
·
Vyakula vya chips chips zenye chumvi
·
Mayai, maharagwe,mikate na mazao ya mahindi
·
Caffeine; umhimize mwenza wako kunywa vinywaji vyenye caffeine
kama koka na pepsi kabla ya kujamiiana kwa sababu vinasaidia kuchangamsha
shahawa Y
·
Kunywa dawa ya kikohozi kabla ya kujamiiana kwa sababu dawa hizo
huwa na guaifenesin inayosaidia nguvu za usafirishwaji wa shahawa
Y. soma juu ya dawa kuhakikiasha ina guaifenesin kabla ya kunywa.
Mambo mengine yanayoweza
kusaidia;
·
Mwanaume afike kileleni/akojoe kwanza.
·
Mwanaume awe juu au akae
·
Mjamiiane huku mmesimama
·
Mjamiiane usiku.
·
Epuka kujamiiana wakati mwezi unatoka au wakati wa mwezi mzima,
fanya mwezi ukiwa robo zaidi.
naomba msaada mm mwezi ulio pita nimeanza ku bleed tarehe6 na huwa nableed kwa cku nne na mwezi huu nimeanza kubleed leo tarehe 30 kwamahesabu hayo mm lini naweza kupata mtoto wa kiume ndani ya mwezi huu cku yangapi
ReplyDeleteAsante kwa maerezo hayohayoooo.������������
ReplyDeletenatamani mungu aje anijalie mtoto wa kiume
DeleteNIME IELEWA HIYO
ReplyDeleteMbona kupata mtoto wa kiume masharti mengi sana
ReplyDeletemie hata sielewi kwa kuwa nyama kahawa soda utajazo vyote ni tindikali. na yai y husafiri zaidi kwenye nyongo ( alkaline)
ReplyDeletealafu siku ulivyozipanga sijaelewa nisaidie hapo
Aki natamani Sana kupata Moto wa kiume,lakini nashindwa kuelewa exactly that date,please help me to know .
ReplyDeleteHii imekaa vizuri Sana.
ReplyDeleteI'aeleweka .
Nafaa kufanya nin ilikupata mtoto wa kiume
ReplyDelete